1 Chronicles 6:27-32

27 aNahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Samweli.

28 bWana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.

29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji Wa Hekalu

31 cHawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

Copyright information for SwhKC